This website uses cookies to ensure you get the best experience on our website.
(WRUA DEVELOPMENT CYCLE) (WDC) – Swahili Version

UTANGULIZI

Uamuzi wa kutafsiri toleo jipya la Nyaraka za WDC katika lugha ya Kiswahili, ulifikiwa kwa lengo la, kwa upande mmoja, kupanua usomaji na matumizi yao hasa katika ngazi za chini kupitia Jumuiya za Watumiaji wa Rasilimali Za Maji (Water Resources Users Associations WRUAs) ambapo ufahamu wa Lugha ya Kiingereza unaweza kuwa haba. Kwa upande mwingine tafsiri hii pia inalenga kutimiza matakwa ya kikatiba kwamba nyaraka za wananchi zinazohusiana na fedha za umma zitolewe katika lugha zote mbili: ya Kiingereza na ya Kiswahili.

Toleo jipya la WDC imeundwa kwa sehemu tatu zinazosaidiana ambazo zimewekwa pamoja katika sehemu tatu tofauti zinazogusia Mfumo, Miongozo ya Uendeshwaji wa Shughuli, na Vifaa Vya Uendeshaji. Mfumo unafafanua mipango ya kazi kati ya WRUAs, WRMA na WSTF kwa masuala ya Mafunzo na ufadhili wa usimamizi wa rasilimali za maji na utawala. Mfumo pia ukiwa na marekebisho kidogo unaweza kutumiwa na wadau wengine wa maendeleo wenye uwezo na nia ya kusaidia shughuli za WRUA katika nchi hii.

Tafsiri hii ya awamu ya kwanza, hata hivyo, haijashughulikia sehemu hizi tatu za WDC lakini inalenga Sehemu ya kwanza kuhusu Mfumo, na sehemu ya pili kuhusu Miongozo ya Uendeshwaji Shughuli, na kuacha nyongeza zinazohusika. Tulizipatia nafasi zaidi sehemu hizi mbili kwa sababu ziko na habari muhimu zaidi na zinalenga kutoa taarifa za utaratibu wa kuundwa kwa WRUA na utekelezwaji wake, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa msaada wa fedha kutoka WSTF. Vifaa vya uendeshaji hutumika kutoa mafunzo kwa wanachama na jamii za WRUA kwa ujumla, juu ya vifungu vya Usimamizi wa Mkusanyiko wa Maji (Catchment Management Strategies CMS) kwa mujibu wa masuala ya Ufanisi wa rasilimali za maji wa mashinani. Katika wakati ujao, na iwapo uwezo utapatikana (WRMA na kiwango cha mashauri) kutumia vifaa vya mafunzo kwa Kiswahili, tunatarajia kutafsiri sehemu zilizobaki ili kuwa na toleo kamili la WDC kwa lugha ya Kiswahili.

Tunatambua na kuzishukuru taasisi na watu waliohusika katika utaratibu wa kutafsiri: hasa tunataka kutoa shukrani zetu kwa Wakala wa Uswisi kwa ajili ya Maendeleo na Ushirikiano (Swiss Agency for Development and Cooperation SDC), kupitia Taaasisi (Centre for Training and Integrated Research in ASAL Development (CETRAD), kwa kufadhili tafsiri hii; timu kutoka taasisi hizi tatu ambazo zilitazama upya na kupangilia vifaa vya kutafsiriwa; na shirika lililotafsiri, na kuunda maandishi, Mtaalamu Mshauri, Muandaaji Nakala kwa Kutumia Kompyuta - Mtandao wa Muundo wa Maandishi Africa, Nairobi (Computer Aided Text Processing Technical Consultant - Africa Typesetting Network Ltd, Nairobi) kwa kazi nzuri waliyoifanya na kuikamilisha kwa muda uliofaa.

Sisi tunahimiza wafanyakazi wa WRMA, wanachama wote wa WRUA, washauri wanaotoa msaada kwa WRUA na kwa wananchi wote, wachukue nafasi ya toleo hili la Kiswahili na kulisoma ili kujifahamisha wenyewe na kuimarisha uelewaji wao kuhusu masharti ya WDC. Hii itasaidia sana kunyorosha malezi na uendeshwaji wa shughuli za WRUA, na hivyo kuboresha utendaji wao na ushawishi wao katika usimamizi wa rasilimali za maji katika maeneo yao wanapoendesha shughuli zao.

Tunawatakia nyote usomaji nzuri na uelewaji wa kina wa dhana ya WRUA.

Pakua Kusoma Zaidi